BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, October 1, 2010

YOUNG DEE ON "TUPO PAMOJA SHOW" THIS FRIDAY..

ARNIE GIZZLE

..............."naitwa Arnie Gizzle........Unataka kujua leo nipo na nani humu ndani?"........... Ni moja ya maneno niliyokuwa najaribu kuzungumza kipindi nafungua show. Hapo kati nimeshatupia vitu zangu kutoka FELIX SINZA CLASSIC WEAR haajah jaah jaah!! nang'aa kama... Nway karibu katika show!!!!!!!!YOUNG DEE

Namwita bwana mdogo kiumri but mkubwa kwa jina, Anaitwa Young Dee!!! Hapa Gizzle na Crew ya Tupo Pamoja ilifanya kumtilia maguu kitaa na kuchonga nae Machache kuhusiana na Muziki wake na nini anafanya kwa sasa na pia tutegemee nini kutoka kwake?.....ARNIE GIZZLE&YOUNG DEE


Unakumbuka ngoma ya Teacher?? iliyopikwa pale kati FishCrab na mtu mzima Lamar... This time Young Dee anakuja na project mpya kutoka Studio ya ukweli pale AUTHENTIC kwa mtu mzima MAX..... Daaaaah humo ndani kuna ngoma moja kali sana inaitwa KIATU....Daaah fanya kutazama show this Friday uwe wa kwanza kuisikiliza haaaaaa haaaaah!!!!!!MAX

Huyu ndio Max wa AUTHENTIC ... Jamaa ni mkali wa sound na Ideas kibao , zaidi ndio mtu anayempa training Young Dee kwa sasa pale kati... Pia ni msaani anayeimba ...... na anazo ngoma kibao na moja ya ngoma zitakazo make headline ni One Minute ambayo kafanya Collabo na Young Dee.... Fanya kucheck show afuu tuoneeeeeeeeee!!!!!!ERASTO MASHINE

Huyu ni mchawi wa Beat anaitwa Erasto Mashine... Anapatikana pale kati AUTHENTIC ndio anafanya mambo yote mle ndani pia ndio mpishi wa track mpya ya Dee Inayotegemea kutoka hivi karibuni...... Unataka kumjua anafanyaje??? Don't miss the show @9pm this Friday Only on Ttv.

Thursday, September 30, 2010

COMING SOON..."LOUD" BY RIHANNA..

LOUD(ALBUM COVER)

Kafanya poa ile mbaya na mzigo uliopita unaitwa "Rated R"..sasa mwanadada anatua mzigo mwingine Nov 12 mwaka huu ambao karibu kila mtu anasubiri kuona itakuwaje??mzigo waitwa "LOUD"....ungojee....

TOMMOROW NI "SUPER FRIDAY" ON THE PEOPLES STATION


Kesho ni "Super Friday" ndani ya Clouds fm "redio ya watu",na hiyo ni katika kusheherekea kitofauti hati ya kuwa super brand radio station iliyotunukiwa na kampuni ya Super Brand International ya nchini Uingereza...so ijumaa ya kesho itakuwa ni ijumaa maalum kabisa kwa redio hiyo kukumbuka ilikotoka kwa kuwaalika na kufanya vipindi walivyokuwa wanafanya wakati wa "struggle" baadhi ya watangazaji  na madj waliowahi kupiga mzigo hapo(wengine bado wapo ila wanafanya shughuli zingine)...baadhi yao ni kama Terrence, Taji Liundi, Ray C, Judith Wambura(JayDee), Fina Mango, Seven, Bobby, ML Chriss, Boggie Master, Jimmy Kabwe, Sakina Lioka, Dj Bonnie Lov, Dj Venture, Dj Mully B, Mr D, Mr C na wengineo ambao wataweza kupatikana...kwa habari kutoka ndani kabisa ya kituo hicho zinasema kesho itakuwa ni siku ya kukumbukwa na ni siku ambayo hakuna msikilizaji atakayetakiwa kuikosa...ni "Super Friday" On the peoples station...

Wednesday, September 29, 2010

UJUMBE WA SKYWOKA KHS HALI YA KIDBWOY...

SKYWOKA

Nilikuwa facebook muda si mrefu nikakutana na ujumbe huu toka kwa SkyWoka..mshkaji na mtu wa karibu zaidi na KidBwoy kwenda kwa fans na friends wote....
"Kwa marafiki zangu wote> Hali ya Kid inaendelea vzr sasa hv. Jana jioni nilienda kumchek nilimkuta amelala. Mama yake alinambia karibu kila mtu anamkumbuka sasa hv na mara nyingi anakuwa na hamu sana ya kuongea lakini kutokana na maumivu ya kichwa haruhisiwi kuongea sana. Ameambiwa ana hitaji utulivu wa hali ya juu. Kwahiyo jamani kwa sasa hatuna tena wasiwasi mkubwa juu ya afya yake. Thnks"
From MNM...
Thanx man Sky...twazidisha maombi ili mshkaji awe fresh soon..na twashukuru pia kwa updates za hali ya Kid pia coz we r so much inlove kwa mshkaji na kwa bht mbaya tuko mbali so inakuwa ngumu kumtembelea ili kujua hali yake...MUNGU NI WETU SOTE...ATATUSAIDIA...ONELOVE!!

Tuesday, September 28, 2010

HONGERENI KWA KUWA "SUPER BRANDY"....CLOUDS FM

Siku zote maisha ni safari ndefu..na mvumilivu hula mbivu...ni safari ngumu ya MAFANIKIO kwa miaka kumi sasa..hongereni kwa kutunukiwa nembo ya SUPER BRANDY fm station..kwenu CLOUDS fm(People's Station)...


Toka enzi hizi...si mchezo manake..ilikuwa ndoto inaotwa ...Zikaja enzi hizi wkt ambapo ndoto imekuwa kweli...timu ya awali kabisa ya 88.4 Clouds fm(1999)And now....guess wat???bata!bata!bata mjini...safari na mafanikio kibao ya mpaka leo kuwa Super Brandy fm station only in Tanzania...hii ni sehemu ndogo tu ya timu kubwa ya Clouds Media wakiwa na mwanaharakati Shy-Rose Banji.