BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, May 4, 2010

HALLE BERRY SAIV NAOMBA IWE ZAMU YANGU BASI...

                               HALLE BERRY WIT DAUGHTER

Hizi ni habari zilizonishtua kidogo na kujiuliza jamani tatizo ni nini??Aliyekuwa mke wa supastaa wa R&B Erick Bennet na mshindi wa tuzo ya Oscar ambaye ni model mkali na mwenye mvuto huko nchini Marekani Halle Berry amepigana chini na jamaa yake wa sasa Gabriel Aubry ambaye pia ni model kutoka Canada.Habari zinasema wawili hao wamemwagana miezi michache nyuma lakini hawakupata nafasi ya kutangaza rasmi.

Chamno kinasema hatua hiyo imetokana na Gabriel kutokuwa na juhudi ya kuyafanya mahusiano ya wawili hao yawe endelevu(usiniulize kivipi) na hivyo Halle Berry kuamua kusitisha malove-dav kwa jamaa japo wataendelea kushiriki kwa pamoja kama wazazi kumlea binti yao "very cute" aliyepatikana enzi za kufana kwa "kuch-kuch hotae" kati yao.Gabriel mwenyewe anasema "sina cha zaidi cha kusema lakini ni wakati mgumu kidogo niliowahi kuupitia,Halle ni mmoja kati ya watu wazuri,wenye upendo,malengo na mvuto niliokwishawahi kukutana nao,imetokea na sasa tuangalie yajayo".Baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na Erick Bennet Halle Berry ndo akawa na jamaa huyu,sasa nani atafuata??naomba iwe mimi basi jamani???.....

0 comments: