BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, August 31, 2010

"AMEJIBU MAOMBI"-UPENDO NKONE..

THE BEAUTIFUL UPENDO NKONE

Baada ya kuishi mjane kwa miaka tisa sasa hatimaye maombi ya mwimbaji maarufu wa muziki wa injili Tanzania UPENDO NKONE ya kupata mume yamejibiwa...Upendo mmoja kati ya wahudumu wazuri nnaowa-admire sasa kufunga ndoa tar 17 mwezi ujao na mchumbake mpya Askofu wa Kanisa la Philadelphia Assembles Kigoma Baba John Mbeyela...."haya ni majibu niliyojibiwa na Baba Mungu Mwenyezi baada ya kuishi maisha magumu na ya upweke kwa muda wa miaka tisa baada ya mume wangu mpendwa kufariki dunia na ndugu wa mume wangu kuinyanyasa sana"..amesema Upendo ambaye hivi sasa yuko safi zaidi kimaisha kwa kufanikisha kupeleka watoto wake international schools, kujenga nyumba nzuri na kuwa na gari zuri la kutembelea baada ya mauzo manono ya albamu zake tatu ambazo ni "Mungu Baba", "Hapa Nilipo" na "Zipo Faida"...Huu ni ushuhuda kuwa AOMBAE HUPEWA..Hongera Upendo Nkone..MNM inakutakia mafanikio katika ndoa yako mpya.

UPENDO NKONE

0 comments: