BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, August 31, 2010

MSALA WA MOZ DEF HUU HAPA..

MOS DEF

Huu ni msala ambao umekuwa ukiripotiwa sana kwenye vyombo vya habari wiki hii...kuwa rappa na mtayarishaji mahiri wa muziki wa Hiphop nchini Marekani Dante Smith aka Mos Def afikishwa kwenye mahakama ya Los Angeles County Superior Court kwa kuitapeli kampuni ya kuandaa matamasha REMG Ent kwa kushindwa kufika kwenye show yao ya Kool Haus huko Toronto Canada ambayo alikwishalipwa malipo ya utangulizi ya dolali za kimarekani 12,500...Moz Def ametakiwa kuilipa kampuni hiyo fidia ya dolali 57,500 baada ya kuisababishia hasara ya maandalizi ya zaidi ya dolali 45,000...so??hii tunajifunza nini???kuwa kumbe hata mbele washkaji wanaingiaga mitini baada ya kupokea kianzio cha show..sio BONGO tu..dah!!

0 comments: