BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, May 14, 2010

MNM's "ALBUM OF THE WEEK" UNTITLED By R-KELLY...

Wiki iliyopita katika album of the week mdau na fans wangu,nilikuwa na CYPRESS HILL na kitu mupya kabisa "RISE UP",hiyo ilikuwa katika HIPHOP naamini ulii-enjoy sana na inawezekana unayo hivi sasa,leo niko katika R&B,tena yule King wao,R-KELLY,na album yake ya sasa "UNTITLED",mpaka sasa jamaa ana singles mbili kali hewani,awali aliachia "ONE" ambayo alimtupia KERI HILSON humo,na sasa ameachia "BE MY NO 2".


Album imeingia mtaani rasmi Septemba 29 mwaka jana chini ya Jive Records & Zomba na ndani ina ngoma 16 kali ambazo zimetengenezwa na R-Kelly mwenyewe na producers kibao kama Lil Ronnie,Gas,Jazze Pha,Infinity,Dj Campa,Los Da Mistro,T-Town Production,Christopher "Deep" Underson,The Pentagon na wengine kibao.Baadhi ya ngoma zilizomo ndani ni pamoja na "Craizy Night" Feat;Rock City, "Text Me", "Exit", "Echo", "Like I do", "Fallin from the Sky", "I Love the Dj", "Elsewhere", "Number One" Feat; Keri Hilson", "Religious" na zingine kibao ambazo siwezi kuzitaja zote hapa.


UNTITLED(ALBUM COVER)

Mdau album hii wiki mbili tu za kwanza ilikimbilia platinum,kama unapenda R&B na SLOWJAMS kama mimi,hii kitu si ya kukosa kabisa,fanya uitafute halafu uone mpango mzima ukoje huko ndani.

0 comments: