BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, June 10, 2010

MTAMBUE HUYU....."TARAJI P. HENSON".

TARAJI PENDA

Ni Taraji P. Henson ambaye alizaliwa Sept 11 1970,wkt nchi yake ikiadhimisha kumbukumbu ya kulipuliwa kwa Trade Centre,yeye mdada anasheherekea birthday yake,ni actress na mwimbaji pia,alizaliwa Northeast Washington DC,mama yake ni Bernice Gordon na baba yake ni Boris Henson ambaye ni US marine na mmiliki wa kampuni yake mwenyewe ya mambo ya fabrication,alilelewa na bibi na babu yake huko Southern Maryland,alisoma Oxon Hill High School na baadae NC A&T ambapo alisomea ufundi umeme na baadae akahamia Howard University,akashinda tunzo ya Triple Threat halafu akaja ku-graduate degree ya Theatre Arts palepale Howard University.


 
KTK POOSE

Taraji ana mtoto mkubwa wa kiume Marcel ambaye alimzaa mwaka 1994.Taraji ameshatokea kwenye muvi kibao tu kama Bad Boy I(2001) "Four Brothers"(2005),"Talk to me"(2007),"Smokin' aces"(2007),"The family that prays" ya Tyra Perry(2008),"Not easily broken"(2009) na "Hurricane season"(2009).Mbali na muvi zote hizo Taraji pia ameshatokea katika michezo kibao ya jukwaani kama "The curious case of Benjamin button" ambapo alitumia jina la Queen na mama yake na Benjamin ambao ulimfanya akawa nominated katika tunzo za Oscar kama "The Best Supporting Actress".Pia ameshafanya vipindi vingi tu vya Tv kama "Lifetime", "The Division" na ABC's "Boston Legal" kwa msimu mmoja.Sio hizo tu pia alitokea kama Angela Scott kwenye ABC's tv show "Eli Stone"(dec 2008),Fox tv show "House"(2005) na CBS's tv show "CSI"(2006),halafu katika episides kadhaa za "Sister,sister".

THE BEAUTY TARAJI

Kimuziki sio kivile sana,ametumbukiza vokoz katika track "Its Hard out here for a pimp" ya Three 6 Mafia,ngoma iliwini Academy Award kama Best Original Song(2006) ambapo pia alipata nafasi ya kuuimba wimbo huo katika kilele cha tunzo za Oscar March 5 2006 akiwa pamoja na washkaji wa Three 6 Mafia,mbali na yote hayo pia Taraji ameshawahi kutokea katika videos za wasanii kibao tu,mfano "Testfy" ya Common(2005),alitokea kama mke wa jamaa aliyetaka kuuawa,pia kwenye "Just like Me" ya Jammie Fox na T.I.Huyu ndio TARAJI PENDA HENSON.MTAMBUE sasa.

TARAJI P. HENSON


0 comments: