BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Monday, May 24, 2010

DIAMOND KUWA MAKINI KWENYE AREA ZA WATU....

Mshindi wa tuzo za Kilimanjaro 2010 Diamond anusurika kupokea kichapo nje ya ukumbi wa st.dominic Iringa baada ya kutaka kumpiga DJ Muba na msanii wa vichekesho Athuman Mussa a.k.a Mwalubadu ambaye pia ni mtangazaji wa Ebony fm Iringa.

DIAMOND AKIPERFOM MISS IRINGA

Diamond alifikia hatua hiyo ya kufanya fujo kubwa katika ukumbi huo baada ya kumaliza kuimba na kushuka jukwani na akiwa nje ya ukumbi huo alimtukana matusi ya nguoni kwa kutumia ishara ya kidole Mbarouk Salum maarufu kama DJ Muba ambaye alikuwa akipiga muziki katika ukumbi huo.


DJ MUBA ON THE 1'N'2

Hatua ya msanii huyu kumtukana DJ Muba ilionyesha kuwakwaza mashabiki wa DJ huyo ambao wamekuwa wakimtegemea katika tasnia ya burudani ndani ya mkoa wa Iringa kwa kupitia kituo cha Radio Ebony Fm na ukumbi wa club V.I.P wa mjini hapo hali iliyopelekea mashabi hao kuanza kumshambulia msanii huyo Diamond kwa kumwita mchanga sana katika sanaa hiyo na kuwa tuzo ya Kilimanjaro isimfanye matawi ya juu pamoja na kumweleza ukweli kuwa DJ Muba ni maarufu mara 100 kwake hivyo asitake kujifanyanisha na DJ huyo kauli zilizomkwaza msanii huyo Diamond.Ebwanaee next time uwe makini area za watu bwana.ohhhooo!!


MWALUBADU.

0 comments: