BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, June 15, 2010

BATA CONTINUES PT II.......

Wadau niko town tayari,nisharudi salama salmini,ila bado kuna mengi kama natakiwa nikupe hivi, yaliyotokea pande zile,baada ya ile kitu ya breakfast pale kati zile time za asubuhi,jioni tukawa na bonge la party pande zilezile za Wilolesi ila this time tukawa Hill Top Hotel.....Ilikuwa ni party ya mtoto aliyefikisha miaka minne(EBONY FM) na kumkaribisha mtoto mpya ambaye ni mdogo wake na huyo mwenye miaka minne bana..(89.5 HOT FM)...unaona uzazi huo??kijani imezingatiwa.....


Huyu ni mmoja kati ya watangazaji mahiri wa Ebony fm ambao wameijenga Ebony kwa kipindi chote cha miaka hiyo minne,anaitwa Agnes Underson Samson aka Mama Kiduchu,"piga nikupige"....


Hapa niko na wadau mbalimbali tukibadilishana mawazo,Mr&Mrs George Ndabagoye pembeni kabisa na mwandishi wa habari maarufu Fransic Godwin.


Mc wa shughuli yenyewe,ni kucheka mwanzo mwisho,anaitwa Athuman Musa Mwalubadu aka King Mwalubadu,pia ni mtangazaji wa Ebony fm...


Hey Mr Deeeeee jaaaaayy!!!!inakuwaje?kama anajiuliza vile nianzejeanzeje,huyu ni Dj mkali mbaya,anaitwa Dj Kwasa,mambo ya Viva Afrika na ishu ka hizo...duh!!mbele ya Pionier...alisababisha mbaya sana...
Mtoto mkali..Juddy Mzurikwao toka 89.5 Hot fm,hapa yuko na Bonnie Zacharia aka Bonnsly..mkuu wa vipindi Ebony fm..wakoshow love na bata zikiendelea..

Hii sekta haikukosekana bana,kama hii siku irudi tena vile.....teh!teh!teh!... Ebony friends pia walikuwa wakutosha tu kama kawa kama dawa,watoto wakali...huyo mwenye blue dah!.sifichi ni mkali,kama nilimu-admire halafu hakushtukia...ilikuwa poa sana...
Shangwe za kutosha na ma-good time kwa kwenda mbele,hapa tukicheza ile yaitwa South African Jive..Aggy akijiachia-achia na mtoto mkali kwa nyuma(hata mkali pia),mbele Juddy wa Hot fm,Bonny na kushoto kwake mimi,nyuma yangu mtu mzima Saggy...saaafiii!!!!


Swaga zikiendelea kunako party,bata ilikuwa poa na ndefu sana wadau,i wish kama irudi tena kesho au keshokutwa hivi....kuna mengi mengine kama nikipata nafasi zaidi ntakuletea japo "uduchu" au vipi,pamoko!pamoko!.... 
 

0 comments: