BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, June 18, 2010

UNTIVIRUS MAMAAAA YANGUUUU!!!!!!KAMA MBELE..


Mamaaa yanguuuu!!!!Hii untivirus hii!!!duh!duh!duh!Mdau na fan wa blog hii ya burudani,yaani nashindwa hata sijui nianzie wapi mimi,aisiii!!!!!Jana jioni nimepata bahati ya kui-download na kuisikiliza kwa makini mixtape hii(Untivirus Vol 1),kwa kifupi naweza sema nawapongeza sana washkaji ambapo kiukweli "wamejitoa mhanga" kwa chochote kitakachotokea,kama ulikuwa hujui,au kama ndio kwanza unaingia kwa mara ya kwanza katika blog hii na labda ndio kwanza unaisikia habari hii ya Untivirus naomba niku-brief kidogo,hii ni project endelevu ya baadhi ya wasanii wakali ambao wameji-organize na kuamua kuutumia muziki huuhuu uliowafanya washine kipindi fulani cha nyuma na kurekodi hii kitu yaitwa untivirus,ni mixtape ambayo inauzungumzia muziki wa kizazi kipya ulivyodidimia na kuwataja kwa majina wale wote ambao inasemekana ndio "mafisadi wa bongo fleva",ndio walioudidimiza muziki huu na kujinufaisha wenyewe,na hii ni vol 1,ikiwa na maana zitakuja zingine kibao,kama nilivyosema hapo awali ni kuwa hawa jamaa wamejitoa mhanga,maana wamezungumza maneno makali na kuwataja kwa majina kabisa wale wote ambao wao wanaamini ndio walioufikisha huu muziki hapa ulipo leo,nimesikia ngoma ya SUGU,mama yangu!!nimesikia ngoma ya MAPACHA,mama yangu!!nimesikia ngoma ya MKOLONI,mama yangu!!asikwambie mtu washkaji wamekuwa very straight foward,hawajapindisha wala kuchengesha chochote,wamesema UKWELI,japo nahisi kuna matatizo makubwa sana yatatokea mbeleni hasa kama waliotajwa katika ngoma zilizomo ndani ya mzigo huo zitawafikia.Kiukweli sitaki kujua ni nini kitafuata,madau mixtape hii inapatikana bure kabisa,so hebu ingia www.ujazo.blogspot.com ya mtu mzima D-7,download halafu sikiliza,mwisho niambie umeionaje??ila.....duh!!!!!

0 comments: