BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Wednesday, June 16, 2010

JOINT YA EBONY FM NA TIMES FM ILIPOWADONDOSHA MAKHIRIKHIRI IRINGA...

Mdau hawa jamaa wanaitwa Makhirikhiri,sidhani kama kuna asiyewafahamu kwa sasa,wanafanya muziki wa kitamaduni huko Botswana,j2 wa wiki iliyopita baada ya zile bata za birthday ya Ebony na kuzaliwa kwa mtoto mpya Hot fm joint tamu ya Ebony fm na Times fm ya Dar akawatupia pale kati Makhirikhiri toka Botswana kwa show mbili kali sana,ya kwanza ilikuwa pale uwanja wa Samora na ya pili ilikuwa pale club VIP.


Huu ni m-stage wetu wa show za nje kama unavyoiona,na hapa mdau stage hii imefungwa kwa size ndogo ya kwanza,yaweza fungwa pia kwa size ya kati na ile kubwa yenyewe,usiipimie kabisa....


Mzigo ulianza kama utani,walianza kama wanatania vile....hapa ni kama wanabeep hivi....


Hapa shughuli imekubali si utani,hawa jamaa kiukweli wanapiga show bana...asikwambie mtu,masaa kama mawili na nusu ya show kali..na hakuna aliyeguna....


Kama kawa watoto wa Ebony walikuwa wamejiachia kwa poose zote backstage,hao ni Leah na Aggy...

0 comments: