FLOETRY
Yap! wanaitwa Floetry,kundi linaoundwa na akinadada wawili wazuri sana,Marsha Ambrosius na Natalie Stewart,kundi ni kutoka London England,tofauti na wengi wanavyodhani kuwa Floetry wame-orign Marekani,wanaimba muziki wa Soul,R&B,Hiphop na Spoken Word Soul.Lebel walikwishafanya nazo kazi ni pamoja na Geffen records na DreamWorks Records,mpaka sasa wana albums tatu,mbili ni za studio na moja ya live.Mdau,namna walivyokuta hawa inashangaza sana,walikutana katika mchezo wa Basketball,Marsha akiwa ni star wa timu yake na Natalie akiwa star wa timu pinzani pia,kwahiyo wakakutana kwenye court,lakini badala ya kuwa maadui wakawa marafiki wakubwa,na katika urafiki huo ndio wakagundua kuwa kumbe pia kila mmoja wao ana ndoto kimuziki,lakini muziki wa aina mbili tofauti,Marsha alilelewa katika mazingira ya kuupenda zaidi muziki wa Reggae wakati Natalie alipenda zaidi muziki wa Funk na Soul.Wakati Natalie akiwa college akisomea mambo ya utumbuziaji,Natalie yeye alikuwa akisomea mambo ya biashara na fedha lakini wakati huohuo walikuwa busy wakijifunza mbinu za sauti na kutumbuiza.
MARSHA & NATALIE(FLOETIC ALBUM)
Walianza rasmi muziki mwaka 1997 ambapo mwaka 2000 walihamia Marekani zaidi kujishughulisha na muziki,na Marsha akapata nafasi ya kuwaandikia watu kibao tu nyimbo kama Jill Scott(nilishamuweka hapa),Jazz wa Dru Hill,Glenn Lewis,Bilal na Michael Jackson katika singo yake ya mwaka 2002 "Butterflies",mwaka 2002 wakasign DreamsWorks Records na wakaachia albam ya kwanza "Floetic" ambayo ndani kuna mikono kibao kama "Floetic","Say Sey" na "Getting Late" ambazo zilifanya vizuri ile mbaya,mzigo pia ulikuja kuachiwa UK ukiwa na nyimbo zingine kadhaa za ziada.Mwaka 2003 wakaachia live album ya kwanza "Floacism" ambayo ilikuwa katika audio cd na dvd,ndani kulikuwa na mkono kama "Wanna be where u are" wakiwa na mkali Moz Def.
FLOETRY
Mwaka 2005 wakaachia mzigo wao wa mwisho "Flo'Ology",mzigo huu ulikuwa mkali kiasi cha kufika mpaka nafasi ya saba kwenye Billboard Top 200 albums,ulipata nafasi ya kuuzwa nakala zaidi ya 77,000 wiki ya kwanza tu toka udondoke kitaa.Mzigo huu ulikuwa wa mwisho kwa "Floetry ya kwanza" kabisa yenye Marsha na Natalie coz baadae mwaka 2007 Natalie alitoka kundini na nafasi ikachukuliwa na demu mkali Amanda Diva na wakapiga bonge la tour mwaka huohuo lakini baada tu ya tour hiyo kundi likasambaratika,baadae Marsha akasign kama msanii wa kujitegemea kwenye lebel ya mtu mzima Dr. Dre "AftarMath Entertainment".Bado hajatoka na solo albam,nadhani yupo katika foleni,lakini keshasikika katika ngoma kadhaa za washkaji kama "The Light" ya Common,"Am Back" ya Styles P,"Start from the schrach" na "Why u hate the Game" za Game,"Get u some" na Cocain" za Nas Escoba na zingine kibao....Hawa ndio FLOETRY....watambue NOW.....
0 comments:
Post a Comment