BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Sunday, June 13, 2010

WADAU BAADA YA KUFIKA BATA ZILIENDELEA HIVI........


Wadau kama kichwa cha habari kinavyojieleza,bata ziliendelea kama kawa,baada ya kufika pande hizo za nyanda za juu kusini cha kwanza kilikuwa ni bonge bonge moja la breakfast kwa mnene wetu maeneo flani ya Wilolesi,nakumbuka mara ya mwisho kugonga breakfast kama hii bana ilikuwa ni miaka kama miwili hivi iliyopita,teh!teh!teh!


Mwenye macho haambiwi tazama bana,si unaona??niko na kaka "mukubwa" Ray pembeni yangu pamoja na Dj Muba,mambo ya "draft",huku kidogo na kule kidogo au vp??


Ukizoea joto la Dar,joto la Iringa we unaona baridi tu hata kama baridi lenyewe hakuna,George Ndabagoye,MNM,Mark Mgeja na Arnie Gizzle mzee wa "Tupo Pamoja",hapo kabla hatujaambiwa "karibuni mezani jamani"


Mambo ya draft yakiendelea,kukutana kama hivi mara chache sana,so ikitokea inakuwa poa sana......


Wana Blog wenzangu,kiukweli nawaaminia sana,J-Ree mzee wa twentyfoursevenmishemishe,waweza mcheki pande zile,katikati Aggy aka kiduchu,waweza pita huko pia nami,sikumbuki tulichokuwa tukikizungumza hapo,ila ni baada ya kushiba sana.


Aaaaaaaa!!!!!Boss!Boss!mbona umejikunyata??baridi nini?lakini wewe si umezoea??teh!teh!ila baridi ya huku haizoeleki bana..kama URUSI.


0 comments: