BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, October 5, 2010

BET HIPHOP AWARDS 2010...NICKI MINAJ STILL SHINING..

NICKI MINAJ(BET HIPHOP AWARDS 2010)

Ishu ilikuwa juzi tu Oct mbili huko Atlanta...ni tuzo za maalum za Hiphop za BET(Black Entertainment Tv) 2010....Jay Z na Nicki Minaj wamesemekana ku-shine ile mbaya baada ya kuzoa tunzo kibao...sasa hapa down tazama washindi kwa ujumla....


*MVP of the yearDrake


*Best Video
Jay-Z and Alicia Keys for “Empire State of Mind”
*Favorite By Fans
Nicki Minaj
*I Am Hip-Hop Award
Salt-N-Pepa
*Rookie of the Year
Nicki Minaj
*Made You Look Style Award
Nicki Minaj
*Perfect Combo Award
Jay-Z and Alicia Keys for “Empire State of Mind”
*Track of the Year(Producer of the year)
Lex Lugar for producing the track “B.M.F.”

Friday, October 1, 2010

YOUNG DEE ON "TUPO PAMOJA SHOW" THIS FRIDAY..

ARNIE GIZZLE

..............."naitwa Arnie Gizzle........Unataka kujua leo nipo na nani humu ndani?"........... Ni moja ya maneno niliyokuwa najaribu kuzungumza kipindi nafungua show. Hapo kati nimeshatupia vitu zangu kutoka FELIX SINZA CLASSIC WEAR haajah jaah jaah!! nang'aa kama... Nway karibu katika show!!!!!!!!



YOUNG DEE

Namwita bwana mdogo kiumri but mkubwa kwa jina, Anaitwa Young Dee!!! Hapa Gizzle na Crew ya Tupo Pamoja ilifanya kumtilia maguu kitaa na kuchonga nae Machache kuhusiana na Muziki wake na nini anafanya kwa sasa na pia tutegemee nini kutoka kwake?.....



ARNIE GIZZLE&YOUNG DEE


Unakumbuka ngoma ya Teacher?? iliyopikwa pale kati FishCrab na mtu mzima Lamar... This time Young Dee anakuja na project mpya kutoka Studio ya ukweli pale AUTHENTIC kwa mtu mzima MAX..... Daaaaah humo ndani kuna ngoma moja kali sana inaitwa KIATU....Daaah fanya kutazama show this Friday uwe wa kwanza kuisikiliza haaaaaa haaaaah!!!!!!



MAX

Huyu ndio Max wa AUTHENTIC ... Jamaa ni mkali wa sound na Ideas kibao , zaidi ndio mtu anayempa training Young Dee kwa sasa pale kati... Pia ni msaani anayeimba ...... na anazo ngoma kibao na moja ya ngoma zitakazo make headline ni One Minute ambayo kafanya Collabo na Young Dee.... Fanya kucheck show afuu tuoneeeeeeeeee!!!!!!



ERASTO MASHINE

Huyu ni mchawi wa Beat anaitwa Erasto Mashine... Anapatikana pale kati AUTHENTIC ndio anafanya mambo yote mle ndani pia ndio mpishi wa track mpya ya Dee Inayotegemea kutoka hivi karibuni...... Unataka kumjua anafanyaje??? Don't miss the show @9pm this Friday Only on Ttv.









Thursday, September 30, 2010

COMING SOON..."LOUD" BY RIHANNA..

LOUD(ALBUM COVER)

Kafanya poa ile mbaya na mzigo uliopita unaitwa "Rated R"..sasa mwanadada anatua mzigo mwingine Nov 12 mwaka huu ambao karibu kila mtu anasubiri kuona itakuwaje??mzigo waitwa "LOUD"....ungojee....

TOMMOROW NI "SUPER FRIDAY" ON THE PEOPLES STATION


Kesho ni "Super Friday" ndani ya Clouds fm "redio ya watu",na hiyo ni katika kusheherekea kitofauti hati ya kuwa super brand radio station iliyotunukiwa na kampuni ya Super Brand International ya nchini Uingereza...so ijumaa ya kesho itakuwa ni ijumaa maalum kabisa kwa redio hiyo kukumbuka ilikotoka kwa kuwaalika na kufanya vipindi walivyokuwa wanafanya wakati wa "struggle" baadhi ya watangazaji  na madj waliowahi kupiga mzigo hapo(wengine bado wapo ila wanafanya shughuli zingine)...baadhi yao ni kama Terrence, Taji Liundi, Ray C, Judith Wambura(JayDee), Fina Mango, Seven, Bobby, ML Chriss, Boggie Master, Jimmy Kabwe, Sakina Lioka, Dj Bonnie Lov, Dj Venture, Dj Mully B, Mr D, Mr C na wengineo ambao wataweza kupatikana...kwa habari kutoka ndani kabisa ya kituo hicho zinasema kesho itakuwa ni siku ya kukumbukwa na ni siku ambayo hakuna msikilizaji atakayetakiwa kuikosa...ni "Super Friday" On the peoples station...

Wednesday, September 29, 2010

UJUMBE WA SKYWOKA KHS HALI YA KIDBWOY...

SKYWOKA

Nilikuwa facebook muda si mrefu nikakutana na ujumbe huu toka kwa SkyWoka..mshkaji na mtu wa karibu zaidi na KidBwoy kwenda kwa fans na friends wote....
"Kwa marafiki zangu wote> Hali ya Kid inaendelea vzr sasa hv. Jana jioni nilienda kumchek nilimkuta amelala. Mama yake alinambia karibu kila mtu anamkumbuka sasa hv na mara nyingi anakuwa na hamu sana ya kuongea lakini kutokana na maumivu ya kichwa haruhisiwi kuongea sana. Ameambiwa ana hitaji utulivu wa hali ya juu. Kwahiyo jamani kwa sasa hatuna tena wasiwasi mkubwa juu ya afya yake. Thnks"
From MNM...
Thanx man Sky...twazidisha maombi ili mshkaji awe fresh soon..na twashukuru pia kwa updates za hali ya Kid pia coz we r so much inlove kwa mshkaji na kwa bht mbaya tuko mbali so inakuwa ngumu kumtembelea ili kujua hali yake...MUNGU NI WETU SOTE...ATATUSAIDIA...ONELOVE!!

Tuesday, September 28, 2010

HONGERENI KWA KUWA "SUPER BRANDY"....CLOUDS FM

Siku zote maisha ni safari ndefu..na mvumilivu hula mbivu...ni safari ngumu ya MAFANIKIO kwa miaka kumi sasa..hongereni kwa kutunukiwa nembo ya SUPER BRANDY fm station..kwenu CLOUDS fm(People's Station)...


Toka enzi hizi...si mchezo manake..ilikuwa ndoto inaotwa ...



Zikaja enzi hizi wkt ambapo ndoto imekuwa kweli...timu ya awali kabisa ya 88.4 Clouds fm(1999)



And now....guess wat???bata!bata!bata mjini...safari na mafanikio kibao ya mpaka leo kuwa Super Brandy fm station only in Tanzania...hii ni sehemu ndogo tu ya timu kubwa ya Clouds Media wakiwa na mwanaharakati Shy-Rose Banji.

Thursday, September 23, 2010

HAYAWI HAYAWI SASA.....KIBOKO CHA ORIGINAL KOMEDI HIKI HAPA...LEO USK

ZE COMEDY SHOW

Leo pale kati show hii inaanza..kupitia "The # 1 youth channel" EATV..washkaji wamesota sana..kwa muda ambao ungekuwa wewe ungeshakata tamaa..ila kuanzia leo ni bata tu coz show ndo itakuwa kwa hewa..tusubiri tuone kama je ni kiboko kweli cha Original Komedi waliokuwa hapa na sasa bata zinaliwa TBC 1??Jibu unalo wewe mwenyewe...

COMING SOON..."PINK FRIDAY" BY NICKI MINAJ

"PINK FRIDAY"(COVER)

Baada ya kugonga copies kibao na mzigo wa kwanza "Massive Attarch"....Nicki Minaj toka lebel ya Young Money sasa anashusha mzigo mwingine matata sana "Pink Friday"...Huu ni mzigo wake mpya kabisa ambao mpaka sasa bado hajatambulisha mkono hata mmoja toka humo ndani...ni juzi tu ndo ametamka rasmi jina la mzigo wenyewe na kutambulisha official cover(kama unavyoona)..Mzigo utadondoka kitaa rasmi Nov 23 mwaka huu..nausubiri ile mbaya..

KIDBWOY AENDELEA VZR..AHAMISHWA WODI..

KIDBWOY

Wadau na fans wengi walitaka kujua mchizi anaendeleaje..baada ya kuripotiwa kuvamiwa na kuumizwa vibaya na mtu asiyefahamika anayesadikiwa kuwa ni msanii....Mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa TETEMESHA Records ambaye pia ni mtangazaji wa Radio Free Africa ya Mwanza Sandu George Mpanda al-maarufu kama KidBwoy kwa sasa hali yake inaendelea vzr..ameweza kuzinduka na kuzungumza japo kidogo baada ya kuwa nusu kaputi kwa zaidi ya masaa 15 baada ya tukio...ila habari mpya zinasema mshkaji imebidi ahamishwe wodi ili kuhepuka usumbufu wa fans kibao ambao daily walikuwa wanajitokeza hospitali ya Bugando alikolazwa kwa nia ya kumjulia hali na kutaka kupigapiga nae stori ishu ambayo madaktari wake wamesema si salama sana kwa sasa coz anahitaji mapumziko zaidi...awali alikuwa wodi no C 606 ghorofa ya sita...kwa sasa amehamishiwa wodi ambayo bado haijawekwa wazi ili apate mapumziko na kuharakisha kupona kwake...Get Well Soon Kid.

HAPPY B'DAY JERMAIN DUPRI...

JERMAIN DUPRI

Mdau leo tar 23 Sept ni siku ya kuzaliwa kwa mmoja kati ya watayarishaji wakali nnaowaaminia wa muziki nchini Marekani Jermain Dupri...so mchizi anasheherekea siku yake leo..kama nawe ni B'day yako leo fahamu kuwa unashea b'day na star huyu...Happy B'day Jermain Dupri..

Tuesday, September 21, 2010

OLD SKOOL....."H-TOWN"...

H-TOWN

F.A NA AMANI NDANI YA B_HITS...

F.A

Habari zinasema mwanamuziki Amani kutoka Kenya wiki hii atatimba ndani ya jiji la Lukuvi kupiga bonge moja la show la East African Bash na wakati huohuo kupata wasaa wa kuingiza vokoz kwenye bongebonge moja la beat la mtu mzima Pancho Latino pale B_Hits ili kukamilisha mzigo mpya wa Hamis Corleone Mwinjuma aka F.A..sasa mimi na wewe tuusubiri tuuone au sio..

AMANI

Thursday, September 16, 2010

HALI YA KIDBWOY WA TETEMESHA RECORDS NA R.F.A NI TETE..

KIDBWOY

Habari zilizonishtua na kuniharibia kabisa siku yangu leo ni hizi...KidBwoy..mtangazaji wa Radio Free Afrika na mmiliki na mtayarishaji muziki katika studio za TETEMESHA RECORDS amevamiwa kwake jana na mtu anayesemekana kuwa ni msanii na kumjeruhi vibaya....ifuatayo ni sms toka kwa mtangazaji na mshikaji wake wa karibu Fredrick Bundala(SkyWoka)..."Kid amevamiwa jana kwake mida ya jioni na mtu anayedhaniwa kuwa ni msanii, amemjuruhi vibaya kwa kumchoma na bisibisi maskioni na kumpiga na kitu kizito kichwani, yuko Bugando Hospital wodi namba C 603 ghorofa ya 6, hali yake si nzuri sana..."...Jamani muziki wetu umefika hapa kweli????Kid get well soon bro...twakuombea,soon utakuwa sawa na kuendelea na kile ukifanyacho kila siku,hii ni kwa niaba ya MNM.

Wednesday, September 15, 2010

ZINANIKUMBUSHA MBALI..."BLACK SUNDAY" BY CYPRESS HILL


Studio album by Cypress Hill
Released July 20, 1993
Recorded 1992-1993
Genre Alternative hip hop, hardcore hip hop, latin hip hop, West Coast hip hop
Length 43:38
Label Ruffhouse
Columbia Records
Producer DJ Muggs
T-Ray
Professional reviews
Cypress Hill chronology
Cypress Hill
(1991)
Black Sunday
(1993)
III: Temples of Boom
(1995)

MNM MEETS...AMINA CHENGO..


NAME;AMINA CHENGO
NICK NAME;EMMY C
BIRTHDAY;MAY 5
OCCUPATION;RADIO PRESENTER
MEDIA;ZENJ FM
CURRENT CITY;ZANZIBAR
HOBBIES;MUSIC,MOVIES&CHILLING

Monday, September 6, 2010

TANGU JANA TAR 06..


Hii mdau imeanza jana kule Arusha...

Arusha International Cultural Diversity Festival (AICDF) 2nd Edition, As planned, this festival will take at three vanues: Alliance Francaise Arusha, WHAT at gallery masai café, Viavia cultural cafe/natural history museum from 6th to 12th Sept 2010.

The main theme of the festival is acknowledging, appreciating, valuing differences and celebrating culture and diversity.
This is a great opportunity for you to explore Arusha and to discover it’s beauty and diversity…huu ulikuwa mualiko wangu but sijapata nafasi ya kuhudhuria...thanx kwa consideration wadau..

VOTE FOR ZUBERI KABWE ZITTO KIGOMA KASKAZINI...

Friday, September 3, 2010

7 YEARZ AGO..SENGEREMA MWANZA..(CHOKA MBAYA RECORDS)

DAW MAJUKANO&RENATUS KILUVIA

Nimeona sio vibaya nikishea nanyi fans wangu..asb ya leo nimepokea simu toka kwa mshkaji wng wa ukweli sana Daw Majukano na kunipa taarifa zilizonishangaza sana...eti blog tuliyoifungua miaka nane iliyopita bado iko hewani mpk leo hii..duh!!Kweli bana..nilipoi-google nikafanikiwa kuifungua na kuiona...aisiii!!kiukweli nimekumbuka mbali sana mdau..hii ilikuwa ni blog ya kuitangaza studio yetu ya kwanza kabisa "Choka Mbaya Records" ambayo tuliifungua na kuanza kufanya kazi ya recording mwaka 2002 Sengerema Mwanza wkt huo tukiwa watangazaji wa kituo cha redio 98.8 fm cha wilayani humo...baadae tulihamisha studio jijini Mwanza na kubadili jina toka Choka Mbaya na kuwa Stonetown Records, halafu Zanzibar(Stonetown I) na Shinyanga(Stonetown II) na mwisho zikaungana mwaka 2007 Kinondoni Dar es Salaam.

STONETOWN RECORDS

Ni safari ndefu ambayo sitakaa niisahau kamwe katika maisha...hapa chini nakuwekea baadhi ya posts tulizoweka kujitambulisha ktk blog hiyo....
"Maelezo kidogo kuhusiana na Studio za CHOKAMBAYA

Choka mbaya records ilibuniwa mwaka 2000. lakini ilianzishwa rasmi mwaka 2003--- december chini ya ma-deejayz wawili ambao ni David james majukano. a.k.a deejay daw na mwenzie Renatus Albinus kiluvia a.k.a rennie bizzo wote wakazi wa jijini Mwanza Tanzania East afrika.CHOKAMBAYA RECORDS ni Studio ya kurekodi muziki aina zote. Neno "chokambaya" linamaanisha kuchoka vibaya( so tired records) hehehehehehe!!! alisema rennie bizzo!! nia na madhumuni ya kuanzisha STUDIO hii na kuisimika jijini mwanza ni kuinua vipaji vya;WASANII chipukuzi wa muziki mbalimbali. kama..HIP-HOP,R&b;b,ZOUK, REGGAE NYIMBO ZA DINI;NYIMBO ZA KITAMADUNI (TRDITIONAL; MUSIC) NK!!! CHOKA MABYA RECORDS ni Studio pekee iliyoko maeneo ya Sengerema na inawakilisha maeneo mbalimbali kwa mfano Geita, mpaka Ngara !!! Dee-jay Daw ni mtangazaji wa radio vilevile ni "PRODUCER" wa "CHOKAMBAYA RECORDS" Rennie Bizzo nae ni mtangazaji na pia ni PRODUCER" ndani ya "CHOKAMBAYA RECORDS"
                      
                    WASANII WOTE MNAKARIBISHWA!!


"Kama wewe ni msanii wa maigizo,muziki wa aina yoyote basi kuwa huru kuwasiliana na sisi .kwa msanii anae toka mbali kidogo na maeneo ya sengerema yaani kwa mfano mwanza city kuja kwetu kurecord atarudishiwa ghalama zake za usafiri na huwa tunawapa kipau mbele sana wansanii kutoka mbali"

Link yenyewe ni http://www.chokambayarecords.8m.com/