BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, April 8, 2010

DNA KWELI UMEOKOKA??AU .........

DnA(kwenye Banjuka Ogopa video)
Mwanamuziki toka Kenya aliyeishtua East Afrika kwa hit "Banjuka" DNA(Dreams And Ambition) ameokoka,kiukweli ni habari njema sana kwangu,na ni habari niliyoifurahia mno,lakini namuuliza DNA "kaka umeokoka kweli?na umeamua kabisa kuachana na kila cha dunia hii?"Najua utajiuliza sana mdau wangu kwanini nimeuliza maswali hayo,sababu ni kwamba,stars wengi wamekuwa wakitangaza kuachana na kila kitu na kuokoka lakini baada ya muda mfupi tumeshuhudia wakirudi dhambini,ni kwanini?sio hapa East Afrika tu,hata Ulaya na Marekani tumeshuhudia hayo,mifano ipo mingi sana,sasa narudia tena DNA kweli umeokoka??hutatuangusha??Wadau na mashabiki wako tupo pamoja nawe na tutakuombea kwa nguvu zote kuhakikisha hurudi nyuma.DNA sasa ametoka na mzigo mkali unaitwa "mtoto wa SONKO"(mtoto wa MUNGU)akiwashirikisha waimba injili maarufu nchini humo Kambua na Issac Kahurah,mzigo ni mkono wa ULOPA na tunamtakia mafanikio katika maisha yake mazuri ya wokovu.

0 comments: