BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, April 6, 2010

THE PLAYER IS BACK!!!

Tiger Woods

Jana katika pitapita zangu kwenye channels za Tv nikagumiana na hii bana,jamaa ambaye miezi kama mitano hivi iliyopita aliuza sana magazeti huko pande za Obama kwa kashfa ya "uplayer"(kutoka na wanawake kibao) star wa gofu Tiger Woods alikuwa live BBC akizungumza na waandishi wa habari.Kikubwa ambacho mshikaji alikuwa anazungumza ni kuhusu ishu yake hiyo."napenda kuomba msamaha kwa fans wangu wote kwa yote yaliyotokea,kiukweli nimekosea sana na imekuwa ni kama funzo kwangu,na tayari yamepita,sitaki kuyapa nafasi tena,kwa sasa natazama zaidi yajayo na naahidi nimejirekebisha na hamtasikia tena chochote kibaya kutoka kwangu,nilikuwa na wakati mgumu sana lakini namshukuru MUNGU yamepita"alisema.Wadau hii ni baada ya miezi mitano ya kutokuzungumza chochote kuhusu kashfa yake hiyo na hajaweka wazi nini anatarajia kufanya juu ya kuparaganyika kwa familia yake kulikotokana na kashfa hiyo,hebu mimi na wewe tutupie macho na masikio yetu pande hizo tuone....

0 comments: