BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Thursday, April 15, 2010

MOSE RADIO&WEASEL TV WITH NEW ALBUM.

Mose Radio&Weasel Tv
Washkaji wanakula sana mashavu na si Kampala tu bali East Afrika na Ulimwenguni kote kwa ujumla.Kwa mfano mwezi May mwaka huu wana show ya kufa mtu Washington DC na mara nyingi wanamuziki toka East Afrika wakipata shows za mbele,juu kwa juu wanapata pia shows zaidi na zaidi na zaidi.Bebe Cool alikwishawahi kuwaponda hawa washkaji,akasema hawezi kutishika na watoto ambao hivi juzi kati alikuwa anawaona kwa macho yake mwenyewe wakiosha magari ya Jose Chamilion,lakini kiukweli mdau wangu tunapokuja kutazama ukali wa mwanamuziki au msanii fulani tunatazama kazi zake na wala si alichokuwa anafanya hapo kabla au sio??
Taaabaaasaaaam!!!!
Sasa sikia hii,washkaji wako tayari kurudi tena kwenu mashabiki na wanachoomba si kingine zaidi ya sapoti ya ukweli ambayo mmekuwa mkiionesha toka walipokuja kwa mara ya kwanza kabisa.Wanakuja na mzigo "mupyaaa" soon,baada ya "Nakudata" ambayo ni albam yao ya kwanza kabisa na "Nyambura" ambayo ilifuata,sasa mzigo mpya uko tayari kabisa,kinachosubiriwa ni kupakuliwa na hiyo itakuwa baada ya show yao ya May huko Washington DC.Sasa hivi vijana hawa wanafanya vizuri na "ability".Mimi nawasubiri,wewe???

1 comments:

Unknown said...

Na mimi nawasubiri pia,I like these guys.