BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, May 28, 2010

MNM'S ALBUM OF THE WEEK..B.O.B presents "THE ADVENTURES OF BOBBY RAY" by B.O.B

Juzi wakati nimeweka alert kuwa ijumaa hii nitakuwa na albam hii,kuna jamaa kanipigia simu akaniuliza nilikuwa wapi siku zote kupreview album ya mchizi huyu??teh!teh!teh!Haya mdau ni ijumaa kama kawa kama dawa,ktk albam of the week tunaucheki mzigo wa huyu mchizi hapa chini.

BOBBY RAY aka B.O.B
                                                    
Mzigo umetoka katika record lebel ya mtu mzima T.I "GRAND HUSTLE RECORDS" na umesimamiwa na Crada,Dr.Luke,The Smeezingtones,Jim Jones,Lil C,Alex da Kid,Polow Da don na Dj Frank E.Exucutive producer ni T.I na rasmi umedondoka kitaa April 27 mwaka huu.Mzigo umeshagonga mpaka namba moja katika Billboards Top 200 album chat na katika wiki ya kwanza tu kitaa watu 84,000 wakajichukulia kopi zao.Single ya kwanza ni "Nothing on You" ambayo iliachiwa Feb 2 na video yake iko nominated ktk category ya video bora ya mwaka kunako BET Awards 2010 na ya pili ni "Airplane" ambayo iliachiwa April 13 bado inasumbua na iko moto vibaya.

COVER ALBUM

Mchizi katumia miaka miwili kuutengeneza mzigo huu na labda ndio maana umeshika sana,sina uhakika na hilo,toka mwaka 2008 mpaka 2010 jamaa alikuwa studio akifanya kazi hii,una urefu wa dk 47 na sekunde 57,cheki mikonozz sasa,kuna "dont let mi fall", "nothing on you" feat;Bruno Mars, "past my shades" feat;Lupe Fiasco, "airplanes" feat;Hayley Williams&Paramore, "bet I" feat;T.I&Playboy Tre, "ghost in the machine", "the kids" feat;Janelle Monae, "magic" feat;Rivers Cuomo of Weezer, "fame", "lovelier than you", "5th dimension" feat;Rico Barino, "airplanes pt II" feat;Eminen&Hayley Williams.

BOBBY RAY

Mdau mimi wiki hii sisemi mengi,fanya hivi utafute mzigo huu halafu utanipa majibu yake,sibahatishi....

0 comments: