BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Tuesday, July 27, 2010

MTAMBUE HUYU..."JOSEPH VAN VICKER"

VAN VICKER

"Mchizi ni raia wa Ghana na alizaliwa Aug 1 1977..mshua wake ni Mdatch na mama yake ni kutoka Liberia..ndo maana ukimcheki fresh mchizi kama kachanganya rangi vile..si ndio??Mshua alifariki mapema sana wakati dogo ana miaka sita tu na kutokana na hilo mchizi akalelewa na mama tu..mpaka leo mchizi anam-appriciate sana mamake na anamuita shujaa wake..kiskuli jamaa kapiga ktk skuli moja yaitwa Mfantsipim.

VAN

Mchizi aliingia kwenye kiwanda cha burudani mwaka 2003 kama mtangazaji wa redio na Tv(Metropolitan Television) na mwaka huohuo akatokea kwenye series moja iliyokuwa ikitengenezwa na kurushwa palepale Ghana "Suncity"..na pale alitumia jina la LeRoy King jr..alicheza kama mwanafunzi wa sanaa aliyezaliwa US na kuja hapo Suncity kumalizia masomo yake..Baada ya kufanya vizuri katika series hiyo Van Vicker akapata mwaliko kama msanii msaidizi katika movie yake ya kwanza "Divine Love" ambamo humo alikutana na wakongwe waliokuwa wakifanya vizuri wakati huo kama Jackie Aygemang na Majid Michael.Ni movie ambayo ilimfungulia milango ktk industry hii huko West Africa..na baada ya hapo ikawa historia..mchizi anakula mashavu ya movies kila kukicha na ameonekana kufanya vizuri zaidi katika soko la Nigeria zaidi kuliko nchini kwake Ghana..amekuwa mkali sana wa romantic movies na ameonekana kuwapiku mghana mwenzake Majid Michael na mnigeria Ramsey Noah.

WITH HIS FAMILY

Kwa wale mademu mnaommezea mimate mchizi huyu hebu sikieni hii..Van Vicker ameoa tyr na ana watoto wawili..kimafanikio mchizi yuko safi mbaya sana..anamiliki kampuni inaitwa Sky & Orange ambayo inadil na matangazo ya biashara na kampuni ingine inaitwa Babetown inayohusika na kuandaa matamasha mbalimbali pale Accra, pia mchizi ana bonge la Unisex Babber Shop ambalo amelipa jina hilohilo la Babetown..mambo ya kijamii pia yumo..anaendesha mfuko unaitwa Van Vicker Foundation ambao unadil na kuinua vipaji mbalimbali vya vijana katika sanaa..huyu ndio Van Vicker sasa..rrrraaaarrruukaaa"!!!

0 comments: