BLOGGER TEMPLATES AND TWITTER BACKGROUNDS

.......

.

Friday, June 18, 2010

UNTIVIRUS MAMAAAA YANGUUUU!!!!!!KAMA MBELE..


Mamaaa yanguuuu!!!!Hii untivirus hii!!!duh!duh!duh!Mdau na fan wa blog hii ya burudani,yaani nashindwa hata sijui nianzie wapi mimi,aisiii!!!!!Jana jioni nimepata bahati ya kui-download na kuisikiliza kwa makini mixtape hii(Untivirus Vol 1),kwa kifupi naweza sema nawapongeza sana washkaji ambapo kiukweli "wamejitoa mhanga" kwa chochote kitakachotokea,kama ulikuwa hujui,au kama ndio kwanza unaingia kwa mara ya kwanza katika blog hii na labda ndio kwanza unaisikia habari hii ya Untivirus naomba niku-brief kidogo,hii ni project endelevu ya baadhi ya wasanii wakali ambao wameji-organize na kuamua kuutumia muziki huuhuu uliowafanya washine kipindi fulani cha nyuma na kurekodi hii kitu yaitwa untivirus,ni mixtape ambayo inauzungumzia muziki wa kizazi kipya ulivyodidimia na kuwataja kwa majina wale wote ambao inasemekana ndio "mafisadi wa bongo fleva",ndio walioudidimiza muziki huu na kujinufaisha wenyewe,na hii ni vol 1,ikiwa na maana zitakuja zingine kibao,kama nilivyosema hapo awali ni kuwa hawa jamaa wamejitoa mhanga,maana wamezungumza maneno makali na kuwataja kwa majina kabisa wale wote ambao wao wanaamini ndio walioufikisha huu muziki hapa ulipo leo,nimesikia ngoma ya SUGU,mama yangu!!nimesikia ngoma ya MAPACHA,mama yangu!!nimesikia ngoma ya MKOLONI,mama yangu!!asikwambie mtu washkaji wamekuwa very straight foward,hawajapindisha wala kuchengesha chochote,wamesema UKWELI,japo nahisi kuna matatizo makubwa sana yatatokea mbeleni hasa kama waliotajwa katika ngoma zilizomo ndani ya mzigo huo zitawafikia.Kiukweli sitaki kujua ni nini kitafuata,madau mixtape hii inapatikana bure kabisa,so hebu ingia www.ujazo.blogspot.com ya mtu mzima D-7,download halafu sikiliza,mwisho niambie umeionaje??ila.....duh!!!!!

Thursday, June 17, 2010

WATAMBUE HAWA..."FLOETRY"...

FLOETRY

Yap! wanaitwa Floetry,kundi linaoundwa na akinadada wawili wazuri sana,Marsha Ambrosius na Natalie Stewart,kundi ni kutoka London England,tofauti na wengi wanavyodhani kuwa Floetry wame-orign Marekani,wanaimba muziki wa Soul,R&B,Hiphop na Spoken Word Soul.Lebel walikwishafanya nazo kazi ni pamoja na Geffen records na DreamWorks Records,mpaka sasa wana albums tatu,mbili ni za studio na moja ya live.Mdau,namna walivyokuta hawa inashangaza sana,walikutana katika mchezo wa Basketball,Marsha akiwa ni star wa timu yake na Natalie akiwa star wa timu pinzani pia,kwahiyo wakakutana kwenye court,lakini badala ya kuwa maadui wakawa marafiki wakubwa,na katika urafiki huo ndio wakagundua kuwa kumbe pia kila mmoja wao ana ndoto kimuziki,lakini muziki wa aina mbili tofauti,Marsha alilelewa katika mazingira ya kuupenda zaidi muziki wa Reggae wakati Natalie alipenda zaidi muziki wa Funk na Soul.Wakati Natalie akiwa college akisomea mambo ya utumbuziaji,Natalie yeye alikuwa akisomea mambo ya biashara na fedha lakini wakati huohuo walikuwa busy wakijifunza mbinu za sauti na kutumbuiza.

MARSHA & NATALIE(FLOETIC ALBUM)

Walianza rasmi muziki mwaka 1997 ambapo mwaka 2000 walihamia Marekani zaidi kujishughulisha na muziki,na Marsha akapata nafasi ya kuwaandikia watu kibao tu nyimbo kama Jill Scott(nilishamuweka hapa),Jazz wa Dru Hill,Glenn Lewis,Bilal na Michael Jackson katika singo yake ya mwaka 2002 "Butterflies",mwaka 2002 wakasign DreamsWorks Records na wakaachia albam ya kwanza "Floetic" ambayo ndani kuna mikono kibao kama "Floetic","Say Sey" na "Getting Late" ambazo zilifanya vizuri ile mbaya,mzigo pia ulikuja kuachiwa UK ukiwa na nyimbo zingine kadhaa za ziada.Mwaka 2003 wakaachia live album ya kwanza "Floacism" ambayo ilikuwa katika audio cd na dvd,ndani kulikuwa na mkono kama "Wanna be where u are" wakiwa na mkali Moz Def.

FLOETRY

Mwaka 2005 wakaachia mzigo wao wa mwisho "Flo'Ology",mzigo huu ulikuwa mkali kiasi cha kufika mpaka nafasi ya saba kwenye Billboard Top 200 albums,ulipata nafasi ya kuuzwa nakala zaidi ya 77,000 wiki ya kwanza tu toka udondoke kitaa.Mzigo huu ulikuwa wa mwisho kwa "Floetry ya kwanza" kabisa yenye Marsha na Natalie coz baadae mwaka 2007 Natalie alitoka kundini na nafasi ikachukuliwa na demu mkali Amanda Diva na wakapiga bonge la tour mwaka huohuo lakini baada tu ya tour hiyo kundi likasambaratika,baadae Marsha akasign kama msanii wa kujitegemea kwenye lebel ya mtu mzima Dr. Dre "AftarMath Entertainment".Bado hajatoka na solo albam,nadhani yupo katika foleni,lakini keshasikika katika ngoma kadhaa za washkaji kama "The Light" ya Common,"Am Back" ya Styles P,"Start from the schrach" na "Why u hate the Game" za Game,"Get u some" na Cocain" za Nas Escoba na zingine kibao....Hawa ndio FLOETRY....watambue NOW.....


OLD SKOOL......"KEITH SWEET"

KEITH SWEET

Katika Old Skool leo nakuletea mchizi ambaye kiukweli nnamiss sana,anaitwa Keith Sweet,mchizi alizaliwa tar 22 July 1961 Harlem New York,huyu ni mwanamuziki wa Urbun,R&B na New Jack Swing,muandishi wa nyimbo,producer na pia ni mtangazaji wa redio.Kabla Keith Sweet hajawa mwanamuziki rasmi alikuwa dalali wa bidhaa New York Mercantile Exchange,lakini baada ya kazi alikuwa anaimba kwenye Night Clubs mbalimbali jijini New York kabla hajaonwa na kusainishwa Elekra Records mwaka 1987.Mpaka sasa Keith Sweet ana watoto wanne,wakike wawili Keysha(1990) na Keia(1992),wakiume wawili pia Jordan(1995) na Justin(1998).Record lebel yake inaitwa Keia Entertainment.

K-S

Kwa sasa jamaa amesign Kedar Records kufanya album yake ya kumi "Ridin" ambayo itatoka June 22 mwaka huu,singo ya kwanza tayari inaitwa "Test Drive" yuko na Joe pia yuko katika lebel hiyo...Huyu ndio Keith Sweet bana,nimemmiss kiukweli.....


HAPPY BIRTHDAY MY YOUNG BRO GEORGE&CRAIZY BONE OF BONE THUGZ N HAMORNY

GEORGE KILUVIA

Leo tar 17 June ni birthday ya mdogo wangu mpendwa ambaye waswahili wanasema "tuliachiana ziwa",yaani baada ya mimi akaja yeye,George Kiluvia Kachenje,miaka kadhaa leo,"sasa dogo mimi napenda nikwambie kitu bana,uko mbali kiukweli,tena sana,so???jitahidi kuishi na watu vizuri huko uliko na ufanye vizuri kile kilichokufanya uwe huko(studies) na hustlings",happy birthday na MUNGU akuzidishie maisha marefu na ufanikiwe kutimiza ndoto zako unazoota kila siku,lakini piiiiiiiiaaaaaaa nataka nikuambie kuwa unashea birthday na superstar na rappa mkali toka kundi la Bone Thugz n harmony,ni Craizy Bone,pia alizaliwa tar kama ya leo miaka kadhaa iliyopita,Happy birthday pia mtu mzima Craizy Bone...

BONE THUGZ N HARMONY


Wednesday, June 16, 2010

HONGERA MSHKAJI WANGU KIZITO BAHATI aka SOSHO..

MR&MRS KIZITO BAHATI

Huyu ni mshikaji wangu wa karibu sana,tumekuwa wote,tumesoma wote na tumecheza wote kitongoji kimoja "Bugando" jijini Mwanza,anaitwa Kizito Bahati aka Sosho ambaye juzi kati ali-tie knock na galfriend wake wa longtime Benadeta Cyril,HONGERA KUBWA kwako kaka,umenionesha njia,pengine nami nianze kufikiriafikiria hilo suala....teh!teh!teh!

KATIKA POOSE

HAWA MBONA WANATUCHANGANYA????

Fans kuna habari ziko kitaa na katika mitandao mbalimbali kuwa Drake na Nicki Minaj wanatoka kimapenzi...lakini mbona ka' ishu hii haieleweki??

DRAKE

Coz Drake kasema alimpenda sana Nicki toka siku ya kwanza anamuona baada ya kukutanishwa na Lil Wayne,na wamekuwa katika uhusiano toka kipindi hicho....

NICKI MINAJ


Wakati huohuo Nicki alipoulizwa akajibu kuwa yeye hana uhusiano na Drake huku akicheka na kutokutoa ufafanuzi zaidi...mbona mnatuchanganya??kama "mnavuvuzelishana" si mseme tu??kwani kuna cha ajabu hapo...aakhhh!!!

TOMMOROW KATIKA "MTAMBUE" HUYU.......FLOETRY

FLOETRY

Kesho hapa kati usiikose hii fans wangu...nitakuwa na wanadada wawili wanaounda kundi la muziki wa Soul "FLOETRY",ni noma...

HAPPY BIRTHDAY 2PAC & FEMI KUTI.....

2PAC SHAKUR

Leo tar 16 June mtu mzima 2Pac Shakur huko aliko anasheherekea siku yake ya kuzaliwa,Pac alizaliwa tar kama ya leo na mwezi kama huu mwaka 1971,alifariki tar 13 Sept 1996 kwa kupigwa risasi,mama yake ni Afeni Shakur,pia tar kama ya leo anasheherekea mwanamuziki toka nchini Nigeria Olufela Olufemi Anikulapo Kuti aka Femi Kuti mtoto wa Fela Anikulapo Kuti,Femi alizaliwa mwaka 1962,mama yake ni Lemi Kuti,so kama unasheherekea birthday yako leo basi tambua unashea birthday na mastaa hawa wawili.

FEMI KUTI

JOINT YA EBONY FM NA TIMES FM ILIPOWADONDOSHA MAKHIRIKHIRI IRINGA...

Mdau hawa jamaa wanaitwa Makhirikhiri,sidhani kama kuna asiyewafahamu kwa sasa,wanafanya muziki wa kitamaduni huko Botswana,j2 wa wiki iliyopita baada ya zile bata za birthday ya Ebony na kuzaliwa kwa mtoto mpya Hot fm joint tamu ya Ebony fm na Times fm ya Dar akawatupia pale kati Makhirikhiri toka Botswana kwa show mbili kali sana,ya kwanza ilikuwa pale uwanja wa Samora na ya pili ilikuwa pale club VIP.


Huu ni m-stage wetu wa show za nje kama unavyoiona,na hapa mdau stage hii imefungwa kwa size ndogo ya kwanza,yaweza fungwa pia kwa size ya kati na ile kubwa yenyewe,usiipimie kabisa....


Mzigo ulianza kama utani,walianza kama wanatania vile....hapa ni kama wanabeep hivi....


Hapa shughuli imekubali si utani,hawa jamaa kiukweli wanapiga show bana...asikwambie mtu,masaa kama mawili na nusu ya show kali..na hakuna aliyeguna....


Kama kawa watoto wa Ebony walikuwa wamejiachia kwa poose zote backstage,hao ni Leah na Aggy...

Tuesday, June 15, 2010

BATA CONTINUES PT II.......

Wadau niko town tayari,nisharudi salama salmini,ila bado kuna mengi kama natakiwa nikupe hivi, yaliyotokea pande zile,baada ya ile kitu ya breakfast pale kati zile time za asubuhi,jioni tukawa na bonge la party pande zilezile za Wilolesi ila this time tukawa Hill Top Hotel.....Ilikuwa ni party ya mtoto aliyefikisha miaka minne(EBONY FM) na kumkaribisha mtoto mpya ambaye ni mdogo wake na huyo mwenye miaka minne bana..(89.5 HOT FM)...unaona uzazi huo??kijani imezingatiwa.....


Huyu ni mmoja kati ya watangazaji mahiri wa Ebony fm ambao wameijenga Ebony kwa kipindi chote cha miaka hiyo minne,anaitwa Agnes Underson Samson aka Mama Kiduchu,"piga nikupige"....


Hapa niko na wadau mbalimbali tukibadilishana mawazo,Mr&Mrs George Ndabagoye pembeni kabisa na mwandishi wa habari maarufu Fransic Godwin.


Mc wa shughuli yenyewe,ni kucheka mwanzo mwisho,anaitwa Athuman Musa Mwalubadu aka King Mwalubadu,pia ni mtangazaji wa Ebony fm...


Hey Mr Deeeeee jaaaaayy!!!!inakuwaje?kama anajiuliza vile nianzejeanzeje,huyu ni Dj mkali mbaya,anaitwa Dj Kwasa,mambo ya Viva Afrika na ishu ka hizo...duh!!mbele ya Pionier...alisababisha mbaya sana...
Mtoto mkali..Juddy Mzurikwao toka 89.5 Hot fm,hapa yuko na Bonnie Zacharia aka Bonnsly..mkuu wa vipindi Ebony fm..wakoshow love na bata zikiendelea..

Hii sekta haikukosekana bana,kama hii siku irudi tena vile.....teh!teh!teh!... Ebony friends pia walikuwa wakutosha tu kama kawa kama dawa,watoto wakali...huyo mwenye blue dah!.sifichi ni mkali,kama nilimu-admire halafu hakushtukia...ilikuwa poa sana...
Shangwe za kutosha na ma-good time kwa kwenda mbele,hapa tukicheza ile yaitwa South African Jive..Aggy akijiachia-achia na mtoto mkali kwa nyuma(hata mkali pia),mbele Juddy wa Hot fm,Bonny na kushoto kwake mimi,nyuma yangu mtu mzima Saggy...saaafiii!!!!


Swaga zikiendelea kunako party,bata ilikuwa poa na ndefu sana wadau,i wish kama irudi tena kesho au keshokutwa hivi....kuna mengi mengine kama nikipata nafasi zaidi ntakuletea japo "uduchu" au vipi,pamoko!pamoko!.... 
 

HAPPY BIRTHDAY MY BEAUTIFUL&LOVELY SISTER...


Ikiwa leo ni tar 15 June,ni siku ya kuzaliwa "my beautiful and very lovely sister" Judith Wambura aka Jide aka Binti Machozi aka Wallet na mengine mengi sana,najua una furaha kupita kiasi,nataka nikwambie kuwa mie pia nimo ndani ya furaha hiyo,twafurahi pamoja,na sina maneno mengi ya kusema zaidi ya haya...."MUNGU azidi kukupa maisha marefu yenye furaha na mafanikio zaidi na zaidi na zaidi,pia uzidi kuwa na moyo huohuo wa upendo na ustahimilivu wa kikwazo chochote kitakachotokea mbele yako"....kwa niaba ya blog ya burudani Muziki Na Maisha na fans wake wote nasema HAPPY BIRTHDAY BINTI MACHOZI...

Sunday, June 13, 2010

UNTI-VIRUS HII HAPA!!!

UNTIVIRUS VOL I

Fans ule mzigo ambao ni project ya mtu mzima SUGU na washkaji wengine kibao "Untivirus" tayari uko kitaa chako kama ulikuwa huna habari sasa mimi nakuhabarisha,ile sehemu ya kwanza ya mzigo tayari iko pande hizo ulipo na kama ukiutafuta naamini utaupata,mzigo unapatika bure kabisa bila gharama yoyote na kwa wale wanaouhitaji na hawako Bongo hii basi ingia http://www.ujazo.blogspot.com/ ili upate nafasi ya ku-download na kuusikiliza,ni project endelevu na tutegemee Vol II soon kwani washkaji kama wako studio hivi wakiendeleza kile wanachokiamini,tusapoti fans.....

WADAU BAADA YA KUFIKA BATA ZILIENDELEA HIVI........


Wadau kama kichwa cha habari kinavyojieleza,bata ziliendelea kama kawa,baada ya kufika pande hizo za nyanda za juu kusini cha kwanza kilikuwa ni bonge bonge moja la breakfast kwa mnene wetu maeneo flani ya Wilolesi,nakumbuka mara ya mwisho kugonga breakfast kama hii bana ilikuwa ni miaka kama miwili hivi iliyopita,teh!teh!teh!


Mwenye macho haambiwi tazama bana,si unaona??niko na kaka "mukubwa" Ray pembeni yangu pamoja na Dj Muba,mambo ya "draft",huku kidogo na kule kidogo au vp??


Ukizoea joto la Dar,joto la Iringa we unaona baridi tu hata kama baridi lenyewe hakuna,George Ndabagoye,MNM,Mark Mgeja na Arnie Gizzle mzee wa "Tupo Pamoja",hapo kabla hatujaambiwa "karibuni mezani jamani"


Mambo ya draft yakiendelea,kukutana kama hivi mara chache sana,so ikitokea inakuwa poa sana......


Wana Blog wenzangu,kiukweli nawaaminia sana,J-Ree mzee wa twentyfoursevenmishemishe,waweza mcheki pande zile,katikati Aggy aka kiduchu,waweza pita huko pia nami,sikumbuki tulichokuwa tukikizungumza hapo,ila ni baada ya kushiba sana.


Aaaaaaaa!!!!!Boss!Boss!mbona umejikunyata??baridi nini?lakini wewe si umezoea??teh!teh!ila baridi ya huku haizoeleki bana..kama URUSI.